Mthokoi

SWAHILI
Asante nyingi kwa Wawuda kwa kutuma mapishi haya kwetu. Nimetayarisha mapishi haya nyumbani mara chache kwa ajili ya familia yangu. Ni mapishi yanayoonekana marahisi sana lakini mchanganyiko wa maharae, mahindi na pilipili mboga/hoho yana utamu mzuri sana ambao unaweza kukufanya uongeze kwenye sahani yako tena na tena. Nafurahi kukwambia haya ni mapishi ya Kenya ambayo ni lazima ujaribu.
Wawuda hakuniambia haya mapishi niya kutoka sehemu gain Kenya, lakini naweza kusema mapishi haya ni kama sawa na Makande ya Tanzania. Tofauti kubwa ni kwamba, Tanzania tunatumia nazi na pia hatuchanganyi na mboga.
Unachohitaji
Mahindi yaliokobolewa kikombe kimoja
Maharagwe kikombe kimoja
Vitunguu viwili
Pilipili Mboga mbili
Saumu kiasi
Nyanya Tatu
Knorr/Royko vijiko viwili
Mafuta kiasi
Upishi wenyewe
- Loweka mahindi kwa mda kwani kawaida huchukua mda mrefu kuiva
- Kisha yachemshe
- Yakishachemka weka maharagwe
- Yape mda wa kutosha yaive pamoja na mahindi
- Vyote vikisha iva epua sufuria yako ili utayarishe viungo
- Pasha mafuta moto hadi yawe moto kabisa
- Weka vitunguu ambavyo vimekatwakatwa
- Vikisha geuka rangi,weka kitunguu saumu ambacho kimepondwa
- Ongeza nyanya ambazo pia zimekatwakatwa
- Pamoja na pilipili mboga
- Ukiwa uko na Royko au knorr bora zaidi,weka vijiko viwili
- Weka chumvi kiasi
- Rojo hili likiwa tayari mimina kwenya sufuria ya mthokoi
- Rudisha tena kwa moto wa chini na ukoroge vizuri vyote vichanganyike
Tayari kupakuliwa.
ENGLISH
Many thanks to Wawuda for sharing this recipe with us. I have prepared this recipe a few times for my family. It seems very simple but the mixture of beans, corn and sweet pepper creates a wonderful flavor that may make you serve this dish again and again. I am happy to tell you this is a must try Kenyan recipe.
Wawuda did not say what part of Kenya this recipe is from; but I can say, it is almost the same as Makande recipe from Tanzania. The main difference is that In Tanzania we add coconut milk and vegetables are served separately.
Ingredients
1 cup Maize (dried)
1 cup Beans (dried)
2 onions
2 green peppers
Any amount Garlic
3 Tomatoes
2 tsp Knorr/Royko
oil for cooking
- Soak dry maize over night and cook next day until well cooked
- Then Boil
- After they boil, add beans
- Simmer until both are cooked
- When cooked remove from heat ad set aside
- Heat oil in pot
- Add chopped onions
- When the onions turn color add chopped garlic
- Add chopped tomatoes
- And then sweet peppers
- Add Roiko or Knorr (two table spoons)
- Add salt
- Simmer, when ready pour in maize and beans pot, mix well
- Simmer mthokoi on low heat until it boils
Serve hot
8 comments July 12th, 2007