Posts filed under 'Vegetables/mboga'

Achali / Pickles

Achali ya KarotiThis is not your regular pickle recipe, but is good enough to satisfy those sudden cravings.
Every country has different recipes for pickles. Majority of those who prepare pickles in Tanzania, prefer to add hot peppers; In Tanzania, pickles must be places in direct sunlight for a week or two before serving, but this is not your regular pickle recipe, because you need only few hours. The best part is, no boiling, no hassles of caring the bottle in an out to the sun for weeks. This is a simple recipe to enjoy with your beer or cocktail. Actually, it is a good vegetable snack.
Karibu

Hii sio achali yako ya kawaida, ni maandalizi yanayoweza kutosheleza hamu yako ya vitu vichachu kwa haraka, na pia ni nzuri kwa afya yako.
Kila nchi ina mapishi yake ya kutengeneza achali. Watu wengi wanaotengeneza achali Tanzania wanapenda kutumia pilipili. Lazima achali iwekwe nje kwenye jua kwa muda wa wiki moja au mbili kabla haijatumika, lakini haya si mapishi ya kawaida kwa sababu unahitaji masaa machache tu. Kitu cha maana ni kwamba, hakuna kupika, ama shida za kubeba chupa ndani na nje kwenye jua kwa muda wa wiki chache. Haya ni maandalizi marahisi kwa ajili ya beer au kokteli. Pia ni kitafunio kizuri sana cha aina ya mboga.
Karibu

Carrots

  • 140g /5 0z Peeled carrots
  • 1/3 cup Vinegar / lime juice
  • 1/3 cup Water
  • 1 tsp Salt
  • 1 tsp Chopped habanera pepper

Cucumber

  • 140g /50z Peeled cucumber
  • 1/3 cup Vinegar / Lime juice
  • 1/3 cup Water
  • 1 tsp Salt
  • 1 tsp Chopped habanera pepper
  1. Cut cucumbers and carrots about four inches long
  2. Arrange the vegetables flat in separate containers.
  3. Add the remaining ingredients in each container.
  4. Cover and let stand for 3 hours.
  5. Remove the liquids and serve.

Good for cocktail and beer.

SWAHILI

Karoti

  • Gramu 140 Karoti zilizo menywa
  • Kikombe 1/3 Siki / maji ya ndimu
  • Kikombe 1/3 Maji
  • Kijiko cha chai 1 Chumvi
  • Kijiko cha chai 1 Pilipili mbuzi zilizo katwa katwa

Matango

  • Gramu 140 Matango yaliyo menywa
  • Kikombe 1/3 Siki / maji ya ndimu
  • Kikombe 1/3 Maji
  • Kijiko cha chai 1 Chumvi
  • Kijiko cha chai 1 Pilipili mbuzi zilizo katwa katwa
  1. Kata matango na karoti kama urefu wa inchi nne.
  2. Panga hizo mboga vizuri kwenye bakuli mbali mbali.
  3. Ongeza viungo vilivyobakia kwenye kila bakuli.
  4. Funika acha viungo vikolee kwa muda wa masaa matatu.
  5. Toa maji, weka mezani.

Ni kitafunia kizuri cha kokteli

12 comments December 19th, 2007


Calendar

August 2008
M T W T F S S
« May    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031

Posts by Month

Posts by Category